April 22, 2013




Hatimaye aliyekuwa mke wa mlipuaji wa bomu katika mashindano ya riadha ya Boston Marathon, Tamerlan Tsarnaev amepatikana.

Mwanadada mrembo, Katherine Russell mwenye umri wa miaka 21 amehojiwa na maofisa wa usalama wa Marekani.

Pamoja naye wazazi wake, baba ambaye ni daktari na mama yake nao walihojiwa kuhusiana na suala hilo.

Katherine alionekana katika nyumba ya zamani ambayo alikuwa akiishi na mlipuaji huyo na walichofanya ni kuingia ndani na kuchukua baadhi ya vitu akiwa amemuacha binti yake Zahara kwenye gari.

 

 

Zahara mwenye umri wa miaka mitatu, alibaki kwenye gari wakati mama yake aliingia na kuchukua baadhi ya vitu kabla ya kurejea na kuondoka.

Inaelezwa ameamua kurudi na kuishi na wazazi wake Rhodes Island baada ya kuona yuko katika wakati mgumu.

Kabla ya hapo Katherine alikuwa mmoja wa wanafunzi wanaocheza dansi katika kikundi cha chuo, lakini baada ya kukutana na mlipuaji huyo alibadilika na kuamua kujitoa.


Tamerlan Tsarnaev..

Pamoja na kubeba ujauzito, aliamua kubadili dini na kuwa mwislamu na akabadili mavazi na kuanza kuvaa hijab na mavazi yanayositili mwili wake tofauti na yale ya utamaduni wa kizungu.

Tamerlan aliuwawa wakati akipambana na  polisi baada ya yeye na mdogo wake, Dzhokhar kugundulika walihusika na ulipuaji wa  mabomu mawili siku ya mashindano ya Boston Marathon jijini Boston, Marekani na watu watatu walipoteza maisha, zaidi ya 100 wakajeruhiwa kati yao 17 vibaya sana.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic