Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo anatarajia kutangaza
wachezaji 30 vijana ambao watawania nafasi ya kucheza katika kikosi cha timu
hiyo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
zimeeleza, Poulsen atatangaza kikosi hicho kesho Jumanne na baada ya hapo timu
hiyo itaingia kambini kwa siku kadhaa.
“Baada ya hapo, Poulsen atakaa kambini na vijana hao kwa siku kadhaa kwa
ajili ya kuhakikisha anapata wengine wachache.
“Nimeambiwa huenda akachagua vijana watano ambao watapewa nafasi ya
kucheza katika kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa.
“Poulsen ambaye amekuwa akifanya mazoezi na vijana hao kwa zaidi ya siku
tano sasa, ameamua kufanya hivyo ili kupata vijana wengine baada ya akina
Kapombe, Msuva kuanza kupata uzoefu,” kilieleza chanzo.
“Kocha anaamini vijana wanatakiwa, hivyo TFF wamekubali kusaidiana naye
ili kumsaidia apate vijana wapya ambao pia watasaidia taifa.
“Kikubwa anachotaka ni vijana wenye vipaji ambao baadaye watakuwa msaada
kwa taifa.”
Poulsen ambaye anaamini vijana, ameifanyia Stars mabadiliko makubwa
katika kipindi chake na kuifanya iwe na kiwango cha kuvutia zaidi.
Kesho saa tano kamili, Poulsen atatangaza majina hayo pamoja na
utaratibu mwingine wa namna kabi itakavyokuwa.








0 COMMENTS:
Post a Comment