Liewig |
Usajili mpya wa timu ya Simba utaanza na wachezaji
kutoka ndani na mchezaji wa kwanza anayetafutwa ni beki wa pembeni.
Baada ya hapo, Simba itafanya kazi ya kusaka beki
wa kati wa uhakika ambaye pia atatokea ndani ya Tanzania.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza
wachezaji wanaotakiwa ni watano lakini Simba imeanza kufanya mchakato wa
wachezaji hao wawili.
“Baada ya hapo, tutaangalia wachezaji wengine kwani
tayari tutakuwa tumepata ripoti ya kocha ya kuacha wachezaji wapi na kuchukua
wa aina ipi” kilieleza chanzo.
Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili
ya Simba, Zacharia Hans Pope alikiri kwamba wanahitaji wachezaji watano au
zaidi lakini watafanya kwa kufuata ripoti ya Kocha, Patrick Liewig.
“Lakini siwezi kuwataja kwa kuwa kila kitu
kinakwenda kwa mpangilio na siri kubwa. Tunataka mambo yaende kitaalamu zaidi.
“Najua mtakuwa mnataka kujua lakini ni vizuri sana
kama mtatupa muda ili tuanze kujipanga na mambo mengi yatafanyika baada ya
mechi ya mwisho dhidi ya Yanga,” alisema Hans Pope.
Simba imeyumba katika msimu huu, hali inayoifanya
kamati hiyo chini ya Hans Pope kuwa na kazi kubwa ya kurekebisha mambo.
0 COMMENTS:
Post a Comment