Wachezaji nyota
wa Ligi Kuu England akiwemo Rio Ferdinand wa Manchester United, wametapeliwa
nchini Morocco.
Ferdinand,
beki wa Chelsea ni kati ya wachezaji wanaokipiga katika Ligi Kuu England
waliokuwa katika ujenzi wa nyumba za kisasa katika moja ya fukwe maarufu nchini
Morocco.
Ujenzi we
nyumba hizo ambao unaelezwa kutarajiwa kugharimu pauni milioni 200 (Sh bilioni
500) ungemalizika mwaka 2010, lakini hadi leo hakuna kilichofanyika.
Wachezaji
hao wawili nyota wakiwemo wawili tena, Garry Neville aliyestaafu na Michael
Carrick ambaye anakipiga Man United walishatanguliza ‘advance’ kwa ajili ya
ujenzi huo, lakini hakuna nyumba hata moja iliyojengwa hadi leo katika eneo
hilo.
Eneo hilo
lingekuwa na nyumba zipatazo 1,342 pamoja na viwanja vitatu vya mchezo wa gofu,
viwanja vya michezo mbalimbali pia.
Terry, Rio
na wenzake wamekuwa wkaitumika katika matangazo ya ujenzi wa eneo hilo maarufu
kama Le Jardin de Fleur katika eneo la Saidia, ili kuwashawishi watu wajitokeze
na kulipa fedha kwa ajili ya kujengewa nyumba.
Wachezaji
hao wameendelea kuwa kimya lakini Mkurugenzi wa Developer Property Logic
inayoshughulikia ujenzi huo, Sean Cusack amesema bado wana imani ya kumaliza
ujenzi huo.
“Hakuna
aliyetegemea kilichotokea, lakini tunaamini mambo yatakuwa mazuri na wanaotaka
nyumba au waliolipia watapa wanachotaka. Tulipata matatizo ya kifedha ambayo
yalitokea dunia nzimba,” alisema.
Inaaminika
mnamo mwaka 2006, Developers Property Logic walikusanya pauni milioni 40 kutoka
kwa waliokuwa wanataka nyumba katika eneo hilo.









0 COMMENTS:
Post a Comment