Leonardo (kushoto) akiwa na Ancelotti, siku alipotua PSG. |
Kocha wa Paris Saint-Germain's (PSG), Carlo Ancelotti ameitwa na uongozi wa Real Madrid akachukue nafasi ya Jose Mourinho anayerejea Chelsea.
Mkurugenzi wa mambo ya soka ya PSG, Leonardo, amesema, Madrid wametuma ombi lao la kumtaka Ancelotti kujiunga nao, lakini Muitaliano huyo ameonyesha anataka kubaki jijini Paris.
“Carlo amepewa ofa na Madrid, wanataka ajiunge nao, lakini yeye ameonyesha anataka kubaki, alilieleza gazeti namba moja la michezo duniani la 'L'Equipe'.
“Kwa upande wa PSG bado tunamhitaji na kama uamuzi wake utakuwa ni kubaki, basi litakuwa ni jambo zuri kwetu,” alisema Leonardo.
Lakini kuna taarifa PSG imekuwa katika mazungumzo na makocha wengine baada ya kuonekana Madrid wameanza kutupa ndoano kwa Ancelotti aliyewahi kung’ara akiwa na AC Milan na baadaye Chelsea.
Real Madrid wamekuwa wakihaha kumsaka mrithi wa Mourinho ambaye
inaelezwa ameshamalizana na Chelsea na mwisho wa mwezi huu utakuwa ni mwisho wa
kazi yake Madrid ambayo anaondoka msimu huu bila ya kuwa na kombe.
0 COMMENTS:
Post a Comment