May 20, 2013



 
Pepe

Kocha Manuel Pellegrini amesema iwapo atatua na kuanza kuinoa Manchester City, usajili wake wa kwanza kabisa anataka uwe wa beki Pepe kutoka Real Madrid.

Pellegrini raia wa Chile amesema Pepe anaamini atamsaidia kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kuwa amewahi kufanya naye kazi.
Pellegrini

Watu wa karibu na Rais wa Madrid, Florentino Perez wamesema wana uhakika bei ya Pepe haiwezi kuzidi euro milioni 25.

Kwake Pepe anaonekana ana furaha akiwa Madrid hasa kwa kuwa Jose Mourinho aliyekorofishana naye mwishoni anaondoka.

Hata hivyo kama Pepe ataamua kubaki na Madrid maarufu kama 'Los Blancos', kocha mpya atakayetua ndiye ataamua kuhusiana na hatima yake na imekuwa ikielezwa Muitaliano, Carlo Ancelotti wa PSG ndiye chaguo la kwanza la Madrid baada ya kuondoka kwa Mourinho.


Bado haijathibitishwa kuhusiana na Pellegrini kutua Man City, lakini ndiye kocha waliyefikia mbali kimazungumzo na chagua la kwanza kwa timu hiyo kuziba pengo la Roberto Mancini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic