Mashabiki Yanga wakimzungusha Ngassa uwanjani mara baada ya mechi dhidi ya Simba kwisha jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. |
Hatimaye Kiungo mwenye kasi, Mrisho Khalfan Ngassa amefunguka na kusema
amesaini Yanga mkataba wa miaka miwili.
Salehjembe ilikuwa ya kwanza kuandika kuhusiana na Ngassa kusaini Yanga
katika mitandao.
Ngassa amezungumza kwa mara ya kwanza na kuthibitisha kwamba kweli
amesaini Yanga.
“Ni kweli nimesaini Yanga, nisingeweza kuzungumzia suala hilo wakati
nina mkataba ambao ulikuwa haujamalizika.
“Lakini baada ya mechi ya mwisho ya ligi, sasa niko huru kuanza
kuutumikia mkataba wangu mpya,” alisema.
Mashabiki wa Yanga walimchukua Ngassa na kumvisha jezi ya njano na
kijani, mara tu baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Yanga na Simba kwenye
Uwanja wa Taifa, jana.
Mashabiki hao walimvisha jezi hiyo na kumbeba na kumbeba na kuondoka
naye hadi nje ya uwanja.
Azam FC ilimpeleka Simba kwa mkopo, lakini Simba imekuwa ikisema
ilimuongezea mkataba wa mwaka mmoja na kumlipa Sh milioni 30 pamoja na gari.
Lakini Ngassa mwenye amekuwa akisisitiza kuwa hana mkataba na Simba kama
ambavyo Wekundu hao wa Msimbazi wamekuwa wakitangaza.
0 COMMENTS:
Post a Comment