May 3, 2013


Big Men..Cheka na Saleh Ally


Baada ya pambano lake dhidi ya Thomas Mashali, bondia Francis Cheka leo alikuwa mitaani jijini Dar es Salaam kuwasalimia ndugu, jamaa na marafiki zake.
 
Cheka akiwa na Mhariri wa Championi Jumatano, Phillip Nkini (kushoto) na mwandishi wa gazeti hilo, Wilbert Molandi 'Baba Andy'..

Moja ya sehemu aliyokuwa amepanga kutembelea ilikuwa ni ofisini kwangu jijini Dar es Salaam, akaniuma sikio kuhusiana na mambo kadhaa yakiwemo yake kuhusiana na pambano lake na Mashali ambalo alishinda kwa KO iliyopatikana kwa konde kali.

Cheka alipita na kuzungumza na mimi, tukajadili mambo kadhaa na kukumbushia enzi zileee…wakati ule na Mhariri wa Championi Jumatano, Phillip Nkini na mwandishi wa gazeti hilo, Wilbert Molandi alikuwa kati ya waliokuwa wakichangia.
 
Still picture na mnato...Saleh, Cheka na Nkini..

Stori zilikuwa nzuri ikiwa ni pamoja na kuzungumzia pambano lake na Mashali lilivyokuwa.

Ingawa Cheka alitoka akiwa safi kabisa katika pambano hilo, lakini amekiri kwamba Mashali ni kati ya mabondia wazuri.

Cheka alisema Mashali si bondia wa kumdharau, alijituma na alifanya kazi yake vizuri, hivyo anampongeza kwa kasi yake nzuri.

“Jamaa ni mzuri, mmoja wa mabondia wajanja sana, ndiyo maana nilikuwa makini.
 
Cheka na Baba Andy...

“Wakati mwingine alikuwa anachea kama ameishachoka hivi, nikiingia anapiga ngumi kali. Nikashtuka, nami nikawa mjanja sana.

“Huenda watu walikuwa wanajiuliza vipi sijammaliza mapema, nilikuwa makini na hali hiyo. Ndiyo maana nasema hakuwa bondia lakini,” anasema Cheka.

Baada ya mazungumzo kwa muda wa kutosha, Cheka aliondoka zake kuendelea kusalimia watu wake kadhaa ‘wa nguvu’, halafu kesho au keshokutwa, ‘atakitoa‘ zake kurejea Morogoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic