Beki Samuel
Ssenkoom wa URA ya Uganda amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea
Simba.
Ssenkoon
anayejulikana kwa jina la Kiboko nchini mwale, amesaini miaka hiyo miwili na
ndiye anachukua nafasi ya Kelvin Yondani ambayo ilionekana haina mwenyewe msimu
uliopita.
Simba
ilianza mazungumzo na beki huyo wiki tatu zilizopita, kabla ya kufikia
makubaliano.
Hata hivyo
taarifa zinaeleza, kutua kwa Ssenkoom, maana yake huenda Mganda mwenzake, Mussa
Mudde akaonyeshwa njia kwa kuwa ameshindwa kufanya vizuri.
Asubuhi na
mapema leo, Salehjembe ilitandaza picha za wachezaji watatu ambao Simba
imewasajili.
Simba
imewasajili Zahoro Pazi, Baba Ubaya na Andrew Ntalla, kipa kutoka Kagera Sugar
ambaye atachukuana kuwania namba na makipa wazoezi katika kikosi cha Simba.
Simba sasa
inahaha kupata mshambuliaji, tayari imezungumza na wawili akiwemo mmoja kutoka
Uganda na mwingine kutoka nchi moja ya Afrika ya Kati.
Simba
imepania kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza msimu ujao ili irejeshe
heshima iliyokuwa imeyumba.
0 COMMENTS:
Post a Comment