Cheka.. |
Bondia Francis Cheka ameonyesha hana mpinzani
katika masumbwi katika kipindi hiki baada ya kumchapa Thomas Mashali.
Cheka kamchapa Mashali katika raundi ya 10 katika
pambano lao la raundi 12 lililomalizika muda mchache uliopita kwenye Ukumbi wa
PTA jijini Dar es Salaam.
Ingawa Mashari alionyesha ushindani mkubwa kuanzia
raundi za mwanzo, kadri muda ulivyokuwa unasonga mbele alishindwa kuhimili
vishindo vya bondia huyo wa Morogoro.
Raundi ya 10, Cheka alimtwanga konde lililompeleka
Mashali ambaye aliona bora shari kamili na kuamua kukubali kwamba amekwisha.
Kutokana na ushindi huo, Cheka amebeba gari aina ya
Toyota Noah ambayo mshindi wa pambano hilo aliahidiwa.
Awali Mashali alikuwa akitamba kwamba yeye ndiye
bondia pekee anayeweza kumchapa Cheka baada ya kuwashinda karibu mabondia wote
wanaojulikana nchini kwa kuwa na uwezo mkubwa.
Lakini imeshindikana na sasa imethibitika kwamba
Cheka, hana mpinzani nchini hasa baada ya kuwapiga lundo la mabondia wakiwemo
wakali kama akina Rashid na Hassan Matumla, Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’,
Karama Nyilawila na wengine kibao.
0 COMMENTS:
Post a Comment