Igboananike |
Ukitaka kujua Wanigeria au
wachezaji kutoka Afrika Magharibi hupania kupata mafanikio wanapopata timu za
kucheza soka la kulipa barani Ulaya tofauti na wale wanaotokea Tanzania, Kennedy
Igboananike anaweza kuwa mfano.
Igboananike raia wa Nigeria
sasa amenunuliwa na AIK Stockholm, moja ya klabu kubwa nchini Sweden na sasa
atakuwa akilamba mshahara wa zaidi ya Sh milioni 10 za Tanzania.
Igboananike aliyezaliwa Februari 26, 1989 jijini Lagos,
Nigeria, aliwahi kucheza kikosi kimoja cha Vasalund ya daraja la kwanza na Mtanzania,
Athumani Machuppa.
Wakiwa pamoja, Igboananike alikuwa analazimika kukaa benchi ili kumpa
nafasi Mtanzania huyo acheze, lakini sasa Igboananike amepiga hatua kubwa na
kununuliwa na klabu hiyo.
Kununuliwa na klabu hiyo
kubwa ni dalili kwamba Igboananike anaweza kupata timu nzuri zaidi katika nchi
zinazolipa kama Italia, Ujerumani, Hispania au England.
Lakini Machuppa anaelekea
kustaafu na mwisho wake katika klabu ya Vasalund haukuwa mzuri sana. Taarifa zinaeleza
yuko nchini, haijajulikana kama ameamua kuachana na soka au atapumzika hadi
msimu ujao.
Salehjembe inaendelea
kujaribu kufanya naye mawasiliano ili kutaka kujua mpango wake kwa kuwa
alipotua Sweden alikuwa mmoja wa washambuliaji wanaokubali ndiyo maana
Wanigeria kama Igboananike walilazimika
kusubiri.
Igboananike alitua Sweden mwaka 2008 na kujiunga na
Vasalunds IF ambako alicheza mismu miwili mwaka 2009 Machuppa alipokuja
Vasalunds if aliwekwa benchi. Mishoni wa msimu 2010 akanunuliwa na Djurgåden
timu kubwa ya premier alikaa misimu miwili mpaka mwaka jana ametula zaidi kwa
kujiunga na AIK Stocholm.
0 COMMENTS:
Post a Comment