Cheka mdogo akishangilia baada ya kutangazwa mshindi dhidi ya Mashali mdogo... |
Wakati
mashabiki walikuwa wanasubiri kwa hamu pambano la Francis Cheka dhidi ya Thomas
Mashali, wadogo zao nao walipewa nafasi katika pambano la utangulizi.
Cosmas Cheka kutoka Morogoro dhidi ya Charles Mashali wa Manzese jijini Dar nao walionyesha
kazi.
Pambano
lao la raundi nane lilikuwa la kuvutia na madogo hao walichapana makonde
vilivyo.
Kila
mmoja alionyesha kumpania mwenzake, walikuwa wakipelekana kwenye kona na
kushambuliana mfululizo.
Kijana
Francis anayetokea katika kambi ya kaka yake, Cheka mwisho aliibuka na ushindi
na wazi ikaonyesha ni utabiri mzuri wa pambano litakalofuata la kaka zao.
Kweli,
ndivyo ilivyokuwa baada ya Cheka kumchapa Mashali kwa KO katika raundi ya kumi
na kumaliza mchezo kabisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment