Kuna taarifa kwamba wagombea
wawili, Jamal Malinzi na Michael Wambura wamerudishwa kuwania nafasi walizokuwa
wakipigania kuzipata katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Taarifa kutoka ndani ya TFF
zimeeleza, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeandika barua ambayo
imeshatua Fifa tayari kuwarejesha Malinzi, Wambura na wengine waliokuwa
wanagombea.
Uongozi wa TFF unatarajia kuzungumza
nusu saa ijayo kuanzia sasa katika ofisi zake katika eneo la Ilala jijini Dar
es Salaam.
Tayari Salehjembe imetega masikio
kuhusiana na kitakachotokea na itawataarifu kama ni hiki kutoka ndani au
kutakuwa na mabadiliko. Endelea kufuatilia.
0 COMMENTS:
Post a Comment