Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetaka
kuanzwa upya kwa utaritibu wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa Shirikisho la Sika
Tanzania (TFF).
Uamuzi huo wa Fifa, maana yake mchakato huo utaanza
upya na unawaruhusu wote walioondolewa awali kama Jamal Malinzi na Michael
Wambura kuwa huru kugombea tena.
Pamoja na hivyo Fifa imeitaka TFF kuanzisha chombo
kitakachoitwa kamati ya maadili na hadhi kwa ajili ya kusimamia mchakato huo.
Awali Fifa ilizuia uchaguzi huo ambao ulipangwa
kufanyika Februari, mwaka huu, baada ya kukumbwa na migogoro, lakini baada ya
kufanya mahojiano na shirikisho hilo, wagombea pamoja na kamati mbalimbali
(Fifa) wametoa maagizo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi punde, Rais wa
TFF, Leodegar Tenga alisema Fifa wamewaeleza kuna kasoro kati zilizojitokeza
huku wakisisitiza kuundwa kwa kamati ya maadili na hadhi kabla ya Oktoba, mwaka
huu.
“Fifa wamesema
kuwa kuna sehemu tulikuwa tunakosea, tunatakiwa kuunda kamati ya maadili na hadhi
ambayo itakuwa na mwanasheria ndiyo tuweze kuendesha uchaguzi huu.
“Wamepatupa muda hadi Oktoba na mchakato wote unaanza
upya, wanaotaka watalipia fomu upya na kila kitu kwa sasa kitakuwa kipya
kabisa,” alisema Tenga.
“Kwa kuwa mchakato utaanza mapema, Fifa wameomba
tutengeneze taarifa ya mambo yanavyokwenda kabla ya Oktoba ili kuokoa muda kabla
ya kufanyika kwa uchaguzi.”
Maana yake, Tenga aliyekuwa amemaliza muda wake zaidi
ya miezi mitano iliyopita, ataendelea kuula katika nafasi hiyo akishughulikia
maandalizi ya uchaguzi.
Uamuzi wa Fifa kuunda kamati hiyo, unaonyesha umelenga
kufanyika kwa mchakato upya, lakini bado inaonekana kutakuwa na ugumu kwa
baadhi ya wagombea kama suala lao litafikishwa katika kamati hiyo ya hadhi na
maadili itakayokuwa imeundwa na TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment