Liewig na Julio wakiwa kazini.. |
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kihwelo maarufu kama Julio alisema Liewig hakutaka kusikia ushauri wake, kitu ambacho kilimfanya hadi akate tamaa.
“Unajua ilifikia watu wakaona kama kocha anahujumiwa, au mimi nafanya makusudi ili asifanikiwe. Lakini ukweli kabisa ni kwamba anakatisha tamaa sana.
URAFIKI WA MASHAKA... |
“Alikuwa hapokei ushauri hata mmoja, alichokuwa anataka yeye basi ndiyo kinakua. Ilifikia wakati nikaanza kukata tamaa kwa kuwa nilikuwepo tu pale.
“Kitu kibaya zaidi kuna tabia ya kuamini kwa kuwa ni mzungu, basi kila anachosema tunaona sawa. Lakini kuna mambo mengi alikosea.
“Sina lengo la kumponda, lakini kweli ilikuwa ni vigumu kufanya naye kazi. Mwisho niliamua kukaa kimya, maana mimi Simba naipenda, hivyo nikaendelea kubaki pale.
“Kweli kama angenisikiliza, basi nakuhakikishia mechi ya kutafutwa bingwa ingekuwa ile ya mwisho wa ligi kati ya Simba na Yanga,” alisema Julio.
Wakati fulani Salehjembe iliwahi kuandika kuhusiana na Julio na Liewig kutokuwa katika maelewano mazuri na ilifikia wakati kocha huyo Mfaransa alikuwa hataki kufanya kazi na Julio.
Lakini makocha hao, wote walikanusha na kusema kila kitu kilikuwa kinakwenda vizuri na hakukuwa na tatizo hadi Julio alipoamua kufunguka leo.
Tayari Simba imemtangaza Abdallah Kibadeni kuwa kocha mpya ingawa Liewig amesema hatambui kufukuzwa kwake kazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment