Nahodha msaidizi wa Real Madrid, Sergio Ramos amesema maneno ambayo yanaonekana wazi kuwa ni dongo kwa kocha wake wa zamani Jose Mourinho.
Ramos amesema kuwa kikosi chao sasa kinahitaji kocha anayewaamini wachezaji badala ya kuwa adui zake.
Ramos amesema maneno hayo huku akiwataja makocha wawili Carlo Ancelotti wa PSG au Heynckes aliyeipa ubingwa wa Ulaya Bayern Munich kuwa ndiyo chaguo sahihi.
Alisema makocha hao wanaoweza kuonyesha tofauti kubwa na makocha wengine ambao wanaweza kuongoza kikosi bila ya kuwaamini wachezaji.
Maneno hayo yanaonyesha kumlenga Mourinho aliyekuwa na mgogoro mkubwa na wachezaji wa Madrid akiwemo Ramos na nahodha Iker Casillas aliyeamua kumuweka benchi kwa zaidi ya miezi mitatu.
Hadi Mourinho anaondoka, alikuwa katika hali ya kutoelewana na Casillas pamoja na beki Pepe raia wa Ureno kama kocha huyo ambaye alijitolea kumtetea kipa huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment