Pazia la Ligi England limefungwa leo huku vita ya nafasi ya tatu na nne
ikipata wenyewe.
Chelsea imefanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuichapa Everton kwa
mabao 2-1 na kufikisha point 75.
Wakati Arsenal iliyokuwa inachuana kwa nguvu na Tottenham, imefanikiwa
kupata nafasi ya nne kwa kuichapa Newcastle kwa bao 1-0 na kufikisha
pointi 73.
Pamoja na Spurs kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland,
imejikuta ikianguka nafasi ya tano kutokana na kuwa na pointi 72, kitu ambacho
kimezua majonzi katika kikosi hicho cha London.
Tayari nafasi ya kwanza ilikuwa na wenyewe Man United ambao mabingwa hao
wamemaliza mechi yao dhidi ya Wes Brom kwa sare ya ‘netiboli’ ya mabao 5-5.
Man City waliokuwa wamejihakikishia nafasi ya pili walilala dhidi ya
Norwich kwa mabao 2-3 wakiwa nyumbani Etihad.
Mechi nyingine, West Ham ikaichapa Reading 4-2, Swansea ikalala kwa
mabao 3-0 dhidi ya Fulham, Liverpool ikaichapa QPR 1-0.
Southampton ikawa 1-1 dhidi ya Stoke, Wigan na Aston Villa wakamaliza na
sare ya 2-2.
Teams
|
P
|
GD
|
PTS
|
|
1
|
38
|
43
|
89
|
|
2
|
38
|
32
|
78
|
|
3
|
38
|
36
|
75
|
|
4
|
38
|
35
|
73
|
|
5
|
38
|
20
|
72
|
0 COMMENTS:
Post a Comment