Pamoja na kutokuwa
katika presha ya kutoteremka daraja au kubeba ubingwa, Ruvu Shooting imepanga
kuichapa Simba katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Mei 5, kwenye
uwanja wa Taifa, Dar.
Msemaji wa Ruvu
Shooting, Masau Bwire amesema wamejiandaa vilivyo na wanazitaka pointi tatu za
Simba.
Ruvu Shooting
inayofundishwa na kocha mkongwe, Charles Boniface Mkwasa imekuwa ni kati ya
timu zinazoonyesha soka la kuvutia.
Tayari iko katika
nafasi ya saba ikiwa na pointi 30 ambazo zinaiweka katika nafasi ya kutokuwa na
hofu ya kuteremka daraja.
“Mazoezi yanaendelea, naweza kusema kama
mandalizi tunajua Simba ni timu ngumu na wanataka nafasi ya tatu, lakini
wasitegemee kutugeuza njia. Sisi pia tunataka pointi tatu,” alisema Masau.
Ruvu Shooting
imekuwa ni kati ya timu zinazoisumbua Simba zinapokutana lakini Mfaransa wa
Simba, Patrick Liewig amesisitiza wanataka kushinda mechi mbili dhidi ya timu
hiyo ya jeshi na ile dhidi ya watani wao Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment