Beki wa kati wa Yang, Mbogo Ladslaus yuko fiti na anaweza akacheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambazo Yanga imebakiza.
Mechi hizo
ni ile ya leo dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa na ile ya Mei 18
dhidi ya watani wao Simba.
Daktari wa
Yanga, Nassor Matuzya amesema tayari amemkabidhi Mbogo kwa Kocha Mkuu, Ernie
Brandts ambaye ataamua kama atampanga au la.
“Sasa Mbogo
yuko fiti na anaweza kucheza, nimeshazungumza na kocha. Hivyo ndiye mwenye
uamuzi wa mwisho kama acheze au la,” alisema.
Beki huyo
wa kati aliyejiunga na Simba akitokea Toto African alifanyiwa upasuaji huo katika
Hospitali ya Mwananyamala ambayo alilazimika kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya
mwezi.
Wiki moja
iliyopita alirejea na kuanza mazoezi na wenzake hadi jana Matuzya aliposema
yuko fiti na anaweza akacheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment