KWA MUJIBU WA RUNINGA YA SUPERSPOT AMBAYO ILIONYESHA LIVE MECHI KATI YA Simba
na Yanga, mechi ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza
watazamaji 57,285.
Mara nyingi, idadi ya watu ambayo hutolewa na SuperSport kama inaonyesha
mechi katika uwanja huo, hupishana na ile ambayo hutolewa na TFF wakati
inatangaza mapato.
Mara nyingi ile ya TFF inakuwa na watu wachache zaidi. Swali kwa sasa, je, TFF watatoa idadi
chache ya watu kama ambavyo imekuwa ikitolewa na kutofautiana na ile ya
SuperSport?
Tusubiri tuone baada ya siku mbili tu!
0 COMMENTS:
Post a Comment