Kiungo mkongwe wa Athumani Idd ‘Chuji’ ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ya watani.
Chuji aliyecheza namba sita katika mechi ya watani leo kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar amekuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Salehjembe limemteua Chuji kuwa mchezaji bora kutokana na uwezo
aliouonyesha lakini SuperSport nayo baadaye ikamtanza Chuji kuwa mchezaji bora
wa mchezo huo.
Chuji aliwathibiti washambuliaji wa Simba na ndiye alikuwa akianzisha
mashambulizi karibu yote ya Yanga.
Chuji alipiga zaidi ya pasi nne ndefu ambazo zilifika, pia alikuwa
akimchezesha kiungo Haruna Niyonzima ambaye pia alimtumia kama sehemu ya
kuhifadhi mipira anapokwama.
0 COMMENTS:
Post a Comment