May 18, 2013



 


Full time, Simba 0 Yanga 2
MWAMUZI ANATIBIWA KWA TAKRIBANI DAKIKA 2, ALIPOINUKA ANACHEZESHA SEKUNDE 42 NA ANAMALIZA MPIRA.


Dk 90*3, Chollo na Kavumbagu wanataka kuzichapa, mwamuzi Saanya anaingilia, bahati mbaya konde linampata na kuchanika juu ya jicho. Mwamuzi yuko chini anatibiwa huku damu zikivuja.
Dk 90*2, Chollo anapiga krosi safi, Singano ndani ya 12, anataka kutoa pasi kwa Sunzu lakini Cannavaro anaiwahi na kutoa pasi kwa Chuji.
Dk 90*1, Ngassa anangushwa, Singano anachonga faulo na Barthez anadaka vizuri.
Dk 87, mashabiki wa Simba wanaanza kutoka nje ya uwanja na Yanga wanazomea kwa nguvu.




Dk 86, Kaseja anasimama na kuendelea baada ya kutibiwa kwa sekunde kadhaa, Yanga wanapiga kona, haina matuna.


 Dk 85, karibu na katikati ya uwanja alipoangushwa Luhende anapiga shuti kali linaokolewa na Kaseja na kugonga mwamba, kona na Kaseja anaemia, sasa anatibiwa
Dk 84, Luhende anawachambua mabeki wanne wa Simba, Mkude analazimika kumuangusha.


Dk 79, Barthez tena anatada krosi kichwani mwa Sunzu ambaye aliruka juu kuiwahi krosi ya Chollo tena.
Dk 78, Barthez anadaka krosi hatua chache kutoka kichwa cha Sunzu, ilikuwa ni krosi nzuri ya Chollo.
Dk 77, Yanga wanafanya mabadiliko, wanamtoa Kiiza anaingia Nizar Khalfan.


Dk 76 Simba wanafanya mabadiliko tena, anatoka Kiemba anaingia Jonas Mkude
Dk 74 Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Chanongo anaingia Ramadhani Singano ‘Messi;.
Dk 66 hadi 70, timu zinacheza zaidi katkati ya uwanja.


GOOOOOO Dk 63, Kiiza anaipatia Yanga bao la pili baada ya mpira wa kurushwa kwa Twite kuwagonga mabeki wa Simba na kumfikia yeye na kuachia shuti kali .
Dk 60, Kiemba anapiga shuti kama mlevi baada ya kupokea pasi nzuri ya Ngassa.
Dk 59, Kiiza anashindwa kuiwahi krosi nzuri ya Msuva, Kaseja anatoka na kudaka.


Dk 56, Kaseja anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa nguvu wa kichwa wa Msuva na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda
Dk 50, Ngassa anapata pasi ya Sunzu, lakini anapiga shuti kuuubwa tena pembeni ya lango
Dk 49, Ngassa anapokea pasi nzuri ya Kiemba, lakini anapiga shuti kuubwa.


Dk 47, Simba wanafanya mabadiliko, anatoka kiungo kinda, Abdallah Seseme, anaingia mshambuliaji Mzambia Felix Sunzu
Kipindi cha pili kimeanza


HALF TIME...Simba 0 Yanga 1

 Possession Simba 42 Yanga 58
Dk 45*2, Kapombe anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa krosi wa Twite na kuwa kona ambayo haikuzaa kitu.
Dk 45*1, Ngassa anauwahi mpira wa krosi uliochongwa na Chollo lakini anautoa mwenyewe, Simba wanamzomea.

Dk 39, Kiiza akiwa anatazamana na Kaseja baada ya pasi nzuri ya Niyonzima, anapiga shuti juuuuu.
DK 37, Simba wanapata kona baada ya krosi Ngassa kuondolewa na Luhende, kona inachongwa na kuwa kona dotto ambayo hata hivyo naizai matunda.

DK 37, Simba wanapata kona baada ya krosi Ngassa kuondolewa na Luhende, kona inachongwa na kuwa kona dotto ambayo hata hivyo naizai matunda.


PENAAAAAT..Dk  26, Cannavaro anamuangusha Ngassa katika eneo la hatari na mwamuzi Saanya anaagiza ipigwe penalty lakini Mussa Mudde anashindwa kufunga. Barthez anaudaka mpira kwa ulahisi kabisa.
Dk 17, Kavumbagu anashindwa kufunga akiwa pekee na kipa Kaseja baada ya krosi nzuri ya Twite.
dk 14 Ngassa anaingia na mpira katika aeneo la hatari lakini Yanga wanaokoa
Dk 6 Pasi nzuri ya Chanongo inamfikia Ngassa lakini Cannavaro anaokoa inakuwa kona isiyozaa matunda.
GOOOO dk  4 Didier Kavambagu anaifungia Yanga bao la kuongoza
KADI YA NJANO:  Dk 1 Mbuyu Twite wa Yanga anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Haruna Chanongo wa Simba.

Gozi linaanza kusukumwa Dimba la Taifa
Simba:
 Juma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba na Haruna Chanongo.
  Sub: Abel Dhaira, Miraji Adam, Ramadhan Singano 'Messi', Felix Sunzu, Christopher Edward, Jonas Mkude na Hassan Mkude.

Yanga:
 Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Athuman Iddi 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima.

Sub: Said Mohamed, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nurdin Bakar, Nizar Khalfan, Said Bahanuzi na Jerry Tegete

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic