Mashabiki wa Man City wameonyesha kuumizwa na uamuzi wa kocha wao wa
zamani, Roberto Mancini kulipia tangazo kwa ajili ya kuwaaga.
Tangazo hilo la kwenye gazeti la Manchester Evening lilipiwa na Mancini
na kuandika ujumbe, “miaka mitatu isiyosahaulika, sitawasahau mashabiki wa
Manchester City. Milele mtabaki moyoni mwangu.”
Halafu kuna picha ya mashabiki, Mancini na ngao ya hisani, makombe ya
Ligi Kuu England na FA.
Mashabiki waliohojiwa na televisheni ya Sky wamesema alichofanya Mancini
ni kitu cha aina yake na imewaumiza kutokana na uungwana kupindukia ambao
haujawahi kufanywa na kocha yoyote nchini humo.
Mancini alitupiwa virago baada ya timu yake kushika nafasi ya pili nyuma
ya mabingwa Man United na Manuel Pellegrin ndiye anaelezwa kuja kuchukua nafasi
yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment