BONDIA Mtanzania Abdallah Pazi, maarufu kama Dulla Mbabe, amemtwanga Mchina, Zulipikaer Maimaitiali kwa TKO katika raundi ya tatu.
Pambano hilo la ubingwa wa WBO Asian Pacif lilifanyika jana nchini China na alishinda kwa TKO raundi ya tatu na kubeba ubingwa wa Super Middle wa WBO Asian Pacific.
Pazi ameshinda Pambano hilo na kukabidhiwa mkanda wake uliokuwa unashikiliwa na Mchina huyo.
Maimaitiali alikuwa anacheza pambano lake la 14 katika ngumi za kulipwa na kabla ya hapo alishinda mapambano mawili mfululizo akitokea kupoteza pambano moja ambalo lilikuwa pekee alilowahi kupoteza.
Mbabe amesema kuwa anarejea Jumatatu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa Mwalimu Nyerere kumpokea.
0 COMMENTS:
Post a Comment