May 7, 2013




Na Saleh Ally
Wajanja Wanigeria wamekuwa wkaitumia jina la kocha wa zamani wa Yanga, Milutin Sredojevich maarufu kama Micho limekuwa likitumika vibaya katika mitandao kwa ajili ya kufanyia utapeli.

Micho pia kocha wa zamani wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini amelaani kitendo hicho na kusisitiza kimelenga kumchafua kwa kuwa anayefanya hivyo si mtu muungwana na kusema kuna kijana wa Kinigeria ndiye amekuwa akifanya hivyo baada ya kufanikiwa kupata namba za siri za email yake na kuanza kufanya uhuni huo.

“Ni kweli, Napata taarifa nyingi sana kwa watu wananiambia kuhusiana na hilo, lakini najua ni kijana mmoja wa Kinigeria ndiye amefanya upuuzi huo.

“Hakika ni kitu kibaya kwa kuwa wanawatumia watu ujumbe na kuwaeleza wanataka msaada wakitumia email yangu na inaonekana mimi ndiye nina matatizo ya fedha.


“Siwezi kufanya hivyo na wala si sahihi hata kidogo, napenda kuwataarifu ndigu na jamaa kwamba mimi niko katika hali nzuri kabisa na sasa niko Addis Ababa, Ethiopia njiani kwenda Rwanda,” alisema Micho, leo.

Sehemu ya ujumbe huo ilikuwa inasomeka hivi:  “Samahani sikukueleza kuhusiana na safari yangu ya London, niko hapa lakini nina matatizo ya kifedha tena niko katika hali mbaya,” ilieleza sehemu ya barua pepe hiyo.

“Tafadhari naomba unitumie kiasi cha fedha ili nijikwamue na ninaahidi kukulipa mara moja baada ya kutoka hapa.”

Kumekuwa na wizi wa kutumia mtandao na watu wamekuwa wakiwatapeli watu wakidanganya kwa kutumia majina ya watu wanaofahamiana nao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic