Msuva (kushoto) na Luhende... |
Na Saleh Ally
Yanga imeingia
katika karne nyingine ya maamuzi baada ya kuwachata mshahara wachezaji wake
wawili, Simon Msuva na David Luhende.
Msuva na
Luhende, kila mmoja amekatwa Sh 200,000 kutokana na kupatikana na hatia ya
kucheza mechi za mchangani maarufu kama ndondo.
Habari za
uhakika kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinaeleza, Msuva na Luhende
‘walijiachia’ na kuchezea timu za mtaani kwao katika michuano ya mchangani kitu
ambacho kimekatazwa na uongozi wa Yanga.
“Ukiachana
na uongozi kukataza, lakini suala hilo liko katika mikataba yao. Unaweza kusema
wamekiunga mikataba, ndiyo maana utaona adhabu imekuwa kubwa ili iwe mfano kwa
wengine.
“Luhende
alikuwa akimlalamikia kocha kwamba fedha alizokatwa ni nyingi sana, lakini
uongozi na hata kocha mwenyewe tumesisitiza adhabu iendelee kubaki hivi,”
kilieleza chanzo.
Ingawa
wachezaji hao hawakutaka kulizungumzia suala hilo, lakini Yanga imeahidi
kupambana na tatizo hilo la wachezaji wake kucheza mechi za mchangani.
Uamuzi huo
unatokana na baadhi ya wachezaji kugundulika huumia wakiwa katika mechi zao
hizo za ndondo lakini klabu inaingia gharama kuwatimu.
Tatizo la
wachezaji kucheza mechi za mchangani kwa ajili ya kujipatia malipo ya ziada
limeendelea kuwa kubwa katika timu mbalimbali za ligi kuu.
0 COMMENTS:
Post a Comment