May 7, 2013



Kocha Mkuu wa Yanga amesema mechi yao na Simba itakuwa ngumu kwa kuwa wapinzani wao hawana cha kupoteza.

Brandts raia wa Uholanzi amesema Simba hawana cha kupoteza kwa kuwa kikosi chao kilishapoteza mwelekeo tofauti na Yanga inayoonekana kuwa timu bora.

“Tayari tuna ubingwa na mambo hayawezi kuwa mazuri kama hatujawashinda Simba, lakini wao hawana cha kupoteza. Hata kama tutawafunga inaweza kuonekana sawa tu.

“Nimewaambia wachezaji wangu tusiwasharau hata kidogo kwa kuwa wana timu nzuri na wanaweza kushindana nasi. Pia hawatakuwa kwenye presha yoyote, hivyo lazima tucheze kwa kutafuta ushindi.

“Hata kama tumekuwa mabingwa, basi lazima tuwafunge Simba katika mechi yetu ya Mei 18 kwa kuwa tuna kikosi kizuri,” alisema Brandts.

Lakini akasisitiza: “Anayedhani itakuwa ni mechi lahisi, basi anafanya makosa makubwa sana. Haiwezi kuwa hivyo, mechi ya wapinzani wa jadi huwa haitabiriki.”


Simba na Yanga zitafunga msimu Mei 18 na Yanga wanataka kushinda ili kuendeleza sherehe ya ubingwa lakini Simba wanataka wapate pointi tatu za kuwapa nafasi ya tatu ili kupunguza makali ya aibu kama watashika nafasi ya nne ambayo inaonekana kugombewa na Kagera Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic