Hii picha ni mwaka 2009, hapa beki
Salum Sued na Kelvin Yondani wakiongozana na madaktari wa Shirikisho la Soka
Afrika (Caf) kwa ajili ya kwenda kuchukuliwa vipimo.
Walikuwa wanachukuliwa vipimo baada ya
mechi za michuano ya Chan iliyofanyika nchini Ivory Coast.
Ilikuwa ni kawaida kila baada ya mechi,
wachezaji wawili wa kila timu wanachukuliwa na jamaa walikuwa wanachagua kwa
vikaratasi.
Maana yake yeyote inaweza kumuangukia,
yaani wachezaji wote wanapewa vikaratasi halafu jamaa wanapita wanakagua.
Kati ya vikaratasi hivyo, viwili ndiyo
vinakuwa na alama na atakayekuwa nacho basi anachukuliwa kwenda kupimwa kama
anatumia dawa za kuongeza nguvu au zile zinazokataliwa michezoni.
Bahati nzuri Sued akiwa Mtibwa Sugar,
Yondani akiwa Simba walikutwa poa na hakuna mchezaji wa Tanzania aliyepatwa na
matatizo hadi tuliporejea nchini salama baada ya kuondolewa na Zambia kutokana
na sare ya bao 1-1 katika mji wa Bouake.
0 COMMENTS:
Post a Comment