Kapombe (kushoto) akiwa kazini... |
Hofu ya Kapombe ni majeraha aliyoyapata katika mechi kati ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast ambayo tayamchelewesha zaidi kwenda Ulaya.
Tayari Kapombe amechelewa takribani siku kumi sasa hali ambayo imezua hofu kwa wakala wake Denis Kadito.
“Kapombe ameomba wiki mbili zaidi kwa kuwa ameumia,” alisema Kadito kutoka nchini Uholanzi.
“Kama itakuwa ni wiki mbili shap, angalau tunaweza kupata nafasi lakini kama atazidi kuchelewa basi tutakuwa hatuna chetu kwa kuwa baada ya wiki mbili klabu zitaingia kwenye program nyingine.
“Unajua bado Tanzania haina jina kubwa katika soka, hivyo inakuwa ni vigumu kidogo kupata nafasi au watu kusubiri.
“Kapombe angeweza kufika mapema, lakini walimzuia kwa ajili ya timu ya taifa, kitu ambacho kimeongeza ugumu.”
Kuhusiana na maendeleo yake, Kapombe alisema anaendelea vizuri na ana matumaini atakwenda Uholanzi mapema angalau awahi majaribio.
0 COMMENTS:
Post a Comment