Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel
Messi amesema hapati muda wa kuangalia soka kupitia kwenye televisheni kwa kuwa
mpenzi wake Antonella hapendi.
Pamoja na hivyo, Messi amesema
Antonella wala kuwa haangalii mechi za Barcelona au Argentina na anaporudi
nyumbani ndiyo humpa matokeo.
“Nikifika humuambia kama nimefunga
mabao mawili au matatu, anakuwa amejua matokeo,” alisema katika mahojiano na
jarida la Corriere della Sera.
“Ninapokuwa nyumbani ninalazimika
kuangalia katuni muda mwingi nikiwa na Thiago (mtoto wake). Nasikia raha kuangalia naye
katuni maana anacheka muda wote tukiwa tunaangalia, nasikia furaha sana.”
Messi yuko katika wakati mgumu kwa kuwa
yeye na baba yake watalazimika kupanda kizimbani Septemba kujibu mashitaka ya
ukwepaji kodi.
Lakini yeye ameahidi siku moja kila
kitu kitapita na atafanya vizuri katika mechi za timu ya taifa na Barcelona
pia.
0 COMMENTS:
Post a Comment