June 25, 2013



Cruyff


Mchezaji nyoya wa zamani wa Barcelona, Johan Cruyff, amesema angekuwa yeye kocha wa timu hiyo, basi asingemsajili nyota Neymari kutoka Brazil.

Au kama angelazimika kumsajili Neymar, akiwa njiani kutua katika klabu hiyo, mara moja angeanza kufanya mipango ya kumuuza nyota Lionel Messi.

Katika mahojiano na gazeti moja la Hispania, Cruyff raia wa Uholanzi aliyewahi pia kuwa Kocha Mkuu wa Barcelona, alisisitiza kuhusiana na suala hilo.

Unafikiri Neymar ataongeza nini kwenye kikosi cha Barcelona?
Tunatakiwa kusubiri tuone, ni mchezaji mwenye kipaji lakini tutaona atacheza vipi na wenzake, hilo ndiyo tatizo.

Kila mmoja anasema hawezi kuelewana na Messi, wewe pia una mawazo hayo?
Kweli pia ninaona hivyo, ingawa ni vizuri wale wanaotoa maoni kama Rosell wakawa na sababu kwa ajili ya ufafanuzi wa kutosha.



Unaona kweli kitendo cha baba yake Neymar kuondoka na euro milioni 40 kwa ajili ya mwanaye kunaweza kusababisha chuki katika chumba cha kubadilishia nguo cha Barcelona?
Ndiyo, inawezekana kabisa, angalia katika mipira ya adhabu, Neymar ni mzuri sana katika kazi hiyo, Messi pia ni bora.

Hiyo ni moja, lakini Messi anadhaminiwa na Adidas ambao ni wapinzani wakubwa wa Nike inayomdhamini Neymar, lazima kuna tatizo litatokea hapa.

Wakati wa kumsajili Neymar, unafikiri ilikuwa vizuri kuachana na Messi?Unakubaliana na hilo?
Neymar akiwa njiani, mara moja ningeanza mipango ya kumuuza Messi, kweli nakubaliana na suala hilo. Ninaamini kutakuwa na ugumu kwa Barcelona katika hilo.


Lakini ni kweli kama wawili hao wakielewana Barcelona itakuwa hatari kupindukia?
Kabisa, wakielewana Barcelona itakuwa tishio, lakini ikishindikana, basi tatizo kubwa kwa Barcelona.

Ungekuwa wewe ndiye kocha, ungeamua kujitolea na kujaribu walichofanya Barcelona?
hapana, hata kidogo. Kikubwa nisingemsajili Neymar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic