June 25, 2013




Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodeger Tenga amesema Tanzania inakuza wachezaji watoto katika mazingira ya soka katika idadi ya chini sana.

Tenga amsema hayo wakati wa kufunga kozi ya makocha waliokuwa wamejitimu leo jijini Dar es Salaam.



“Tunakuza idadi ndogo sana ya watoto, wenzetu wana idadi kubwa sana hivyo tunalazimika kuongeza mambo mengi muhimu.


“Suala la kuwa na makocha wenye mafunzo kama hivi ni zuri na la muhimu. Lakini bado juhudi kubwa inatakiwa na hili si tatizo la Tanzania pekee, ni Afrika nzima,” alisema Tenga.

“Angalia, mfano Ujerumani wachezaji wanaofuatiliwa wakiwa chini ya uangalizi mzuri wanafikia milioni. Maana yake wana uhakika wa kufanya vizuri zaidi. Hili lazima tuliangalie.”

Aidha, Tenga ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga, Pan African na timu ya taifa alionya kuhusiana na wachezaji wengi kubweteka kutokana na mafanikio kiduchu wanayoyapata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic