Uongozi wa Yanga umesema hautakwenda kupokea zawadi ya ubingwa ambayo wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom wamesema wataitoa Julai 3.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema wameamua kutokwenda kupokea zawadi hizo na wanaamini Vodacom watazipeleka kwao.
Kizuguto amesema walitarajia kupewa zawadi hizo tokea Mei 18, lakini haikuwa hivyo na Vodacom wameendelea kuchelewesha zawadi hizo.
“Hii ni mara ya tatu wanatangaza, maana walianza kutanga mara ya kwanza, wakaahirisha, mara ya pili pia ikawa hivyo.
“Tunaona hatutaenda kabisa, maana wamechelewesha kila kitu na hawakuwa na sababu za msingi kufanya hivyo,” alisema Kizuguto na kuongeza.
“Tunajua hata kama hatutaenda, basi huo ndiyo uamuzi wetu na tunajua zawadi zetu tutapata kwa kuwa tunastahili.”
Wiki iliyopita, Vodacom walitangaza siku hiyo maalum kwa ajili ya kuwakabidhi washindi na wachezaji bora wa ligi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment