Thiago akiwa na Neymar ambaye tayari ametua Barca.. |
Tayari Barcelona
wameanya kazi ya kuhakikisha wanapata mrithi wa beki wao mkongwe, Carles Puyol
ambaye umri na majeruhi vimepunguza uwezo wake.
Barcelona imepanga
majina ya mabeki tisa kutoka timu mbalimbali za Ulaya ingawa chaguo la kwanza
linaonekana kuwa ni Thiago Silva wa PSG.
Pamoja na
Thiago, Barcelona pia imewalenga Hummels (Dortmund), Kompany na Lescott (City),
Marquinhos (Roma), David Luiz and Ivanovic (Chelsea), Ínigo Martínez (Real
Sociedad) na Vermaelen (Arsenal).
Lengo la
Barcelona ni kuwa na beki imara kwa kuwa msimu uliopita, safu yake ya ulinzi
ilionekana kuyumba, kitu ambacho hawataki kitokee msimu ujao.
Suala la Thiago
ambaye amepewa nafasi ya kwanza na Kocha Mkuu, Tito Vilanova litategemea bei
kutoka kwa PSG, kama itakuwa juu sana, basi Barcelona wataanza kuangalia mabeki
wengine kwa kufuata listi yao.
0 COMMENTS:
Post a Comment