Kocha Carlo
Ancelotti ameonyesha kukerwa na tabia ya uongozi wa PSG kuonyesha unataka
kumbakiza.
Ancelotti raia
wa Italia amemuambia rafiki yake wa karibu aliyezungumza na gazeti la Le Parisien
la Ufaransa kwamba anataka kwenda Madrid lakini PSG wanaonekana kutaka
kumlazimisha kubaki.
Kocha huyo wa
zamani wa AC Milan na Chelsea amesema Rais wa PSG, Nasser Al Khelaifi amekuwa
akitaka kulazimisha abaki lakini yeye anataka kuondoka.
Rafiki yake huyo
amesemma tayari Ancelotti ameshafuta mawazo ya kubaki PGS na anataka kuendelea
mbele na Madrid ndiyo ndoto yake kwa kuwa pia inamhitaji kuchukua nafasi ya
Jose Mourinho aliyerejea Chelsea.
0 COMMENTS:
Post a Comment