Mtanzania Yona
Ndabila amekumbana na balaa kwa kulambwa kadi nyekundu ikiwa ni mechi nne tu
baada ya kuichezea timu yake mpya.
Ndabila awali
alikuwa akiichezea Saraswoti Youth Club kwa takribani misimu mitatu kabla ya
kujiunga na Manang FC ambayo ni moja ya timu kubwa nchini Nepal
“Kweli
nimepigwa kadi nyekundu, sikutegemea na ilikuwa ni hali ya kawaida tu ya mchezo
lakini huenda mwamuzi hakuelewa.
“Lakini
hakuna kitu kibaya, naendelea kupambana kwa ajili ya kuhakikisha naisaidia timu
yangu. Kipindi nitakachokuwa nje kutokana na adhabu hiyo nitaendelea na mazoezi
kwa juhudi,” alisema Ndabila.
Akiwa nchini
Ndabila aliwahi kung’ara na Prisons ya Mbeya pamoja na Mtibwa Sugar ya Morogoro
lakini baadaye aliamua kutoka nchini na kwenda nje kutafuta maisha.
Wakati akicheza
soka nchini, Ndabila aliwahi kuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa katika kikosi
cha Stars chini ya Marcio Maximo ambacho kilisafiri na kwenda kucheza mechi ya
kirafiki nchini yemen.








0 COMMENTS:
Post a Comment