Mshambuliaji Edinson Cavani ameweka wazi kwamba angependa kufundishwa na
makocha wawili.
Cavani raia wa Uruguay amewataja makocha hao kuwa ni Jose Mourinho au
Manuel Pellegrini.
Maana yake, Cavani amechagua kuhamia Ligi Kuu England kwa kuwa makocha hao
wote watakuwa England.
Mourinho ameishatua Chelsea na Pellegrini anaonekana kuwa mali ya
Manchester City.
“Bado nina mkataba na Napoli, lakini ninazungumza na klabu nyingine,
makocha hao wawili ningependa kufanya kazi na mmoja wao,” alisema.
Alipoulizwa kuhusiana na Real Madrid, akajibu, “sina uhakika, kila mtu
angependa kucheza La Liga, lakini bado sijajua mwisho wangu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment