Siku moja tu baada ya kiungo nyota wa Barcelona, Andres Iniesta kutamka
kwamba Kocha Jose Mourinho alichangia kuua soka la Hispania, kocha huyo
amejibu.
Mourinho aliyekuwa kocha mkuu wa Real Madrid amesema anakubaliana na
Iniesta kwamba aliua soka la Hispania kwa kuwa alivuruga tabia za Barcelona
kuwa timu isiyofungika.
“Kweli kama kuondoa utawala wa Barcelona kuwa timu isiyowezekana ni kuua
soka la Hispania, basi yuko sahihi.
“Kwa mtu anayefuatilia atakuwa na majibu, kwamba Barcelona ilionekana ni
timu isiyofungika na walijua kila kitu.
“Hata mimi mwanzo nilifungwa mabao matano, lakini nilituliza akili na
kujipanga, baadaye waulize, kazi yangu wanaijua hivyo kama hivyo ni kuua soka,
basi sawa.”
Jana Iniesta alimshambulia Mourinho na kusema amevuruga na kuporomosha soka
la Hispania, lakini bado ilionekana pia kauli yake ililenga kumtetea rafiki
yake Iker Casillas aliyekuwa na ugomvi mkubwa na Mourinho.
0 COMMENTS:
Post a Comment