Wachezaji
nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa, Frank Riberry na Karim Benzema wamefikishwa
kizimbani kutokana na kupata huduma ya changudoa mwenye umri mdogo.
Changudoa
huyo aitwaye Dehar mwenye asili ya Algeria amesema wachezaji hao walijua ana
umri mdogo lakini bado walikubali kupata huduma yake.
Imeelezwa
Riberry ambaye anakipiga Bayern Munich alipata huduma ya Dehar wakati akiwa na
miaka 17.
Dehar
ameileza mahakama kuwa Riberry alimlipia ndege na kumsafirisha hadi Munich
ambako kulikuwa na sherehe yake ya kuzaliwa na ‘akamtumia’ mwisho akampa ujira wa
euro 700 tu.
Lakini
changudoa huyo dogodogo amesisitiza hata Benzema anayekipiga Real Madrid alimtumia
pia wakati akiwa na miaka 16 huku akijua ni makosa.
Wote
wawili wamekanusha ingawa Riberry amesema amewahi kumjua Dehar na aliwahi pia
kumlipia euro 200 kwa ajili ya taxi na si zaidi.
Wachezaji
hao nyota hawakutokea mahakamani na badala yake waliwakilishwa na wanasheria
wao.
Kwa
mujibu wa sheria za Ufaransa, iwapo watapatikana na hatia, basi watahukumiwa
kwenda jela miaka mitatu au faini ya euro 40,000.










0 COMMENTS:
Post a Comment