Pamoja na kuwa msumari wa
moto kwa mabeki wa Tanzania, mshambuliaji wa Arsenal, Gervinho amezua gumzo
kutokana na tabia yake ya kukosa mabao ya wazi.
Mashabiki wengi wa Arsenal
wamekuwa wakilaumu kuhusiana na mchezaji huyo kupoteza nafasi za wazi katika
mechi za Ligi Kuu England.
Katika mechi ya juzi dhidi
ya Taifa Stars, Gervinho alikuwa moto wa kuotea mbali wakati akiichezea Ivory
Coast kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Lakini moja ya kitu
alichofanya na kusababisha mjadala huo ni kukosa bao la wazi akiwa amebaki yeye
na kipa Juma Kaseja.
Gervinho aliwazidi mbio
mabeki wa Stars, Nadir Haroub Cannavaro na Kelvin Yondani, baada ya kubaki na
Kaseja, alipiga mpira dhaifu ambao ulikwenda moja kwa moja kwenye mikono ya
kipa huyo.
Ingawa wengi walifurahi
kutokana na kukosa kwake, lakini mashabiki wengi wa soka la England walianza
kumjadili.
Katika baadhi ya mitandao
wamemuelezea kama mchezaji hatari katika suala la kusumbua na kupiga krosi
lakini si kufunga.
Gervinho ni kati ya
wachezaji wanaopoteza nafasi nyingi sana za kufunga akiwa katika nafasi nzuri
ya kufanya hivyo.







0 COMMENTS:
Post a Comment