June 19, 2013




Vijana wa timu ya soka ya Hispania chini ya miaka 21 wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara nyingine tena.

Vijana hao wamechukua kombe hilo baada ya kuwachapa Italia kwa mabao 4-2 katika mechi kali ya kusisimua.


Hispania ilikuwa timu bora tokea mwanzo wa mashindano hayo na Thiago Alcantara wa Barcelona alifunga mabao matatu kati ya hayo manne na moja likipachikwa kimiani na Isco. Mechi hiyo ilipigwa kwenye Uwanja wa Teddy mjini Jerusalem.


Kwa ushindi huo, maana yake Hispania inaendelea kuwa mbabe wa soka duniani bila ya kujali ni vijana au timu kubwa.

Soka lao lilikuwa na kuvutia tokea mwanzo wa mashindano na ilikuwa lahidi kutabiri kwamba wangekuwa mabingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic