Na Saleh Ally
KIUNGO nyota we Ivory Coast, Yaya Toure
ameendeleza vituko na misimamo baada ya kugoma kushuka kwenye ndege wakati
wakiwa njiani kurejea jijini Abidjan.
Baada ya mechi dhidi yaTaifa Stars, Tembo hao
walielekea moja kwa moja kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
na kuanza safari ya kwenda kwao Ivory Coast.
Wakiwa njiani, ndege hiyo iliteremka katika mji
mkuu wa Benin uitwao Porto-Novo ambako
walikodi ndege hiuo, lengo lilikuwa ni kuweka mafuta.
Lakini mmoja wa mawaziri wa serikali ya nchi
hiyo ambaye alipewa taarifa Ivory Coast watapita hapo, aliomba wachezaji na
viongozi washuke na kuingia kwenye cchumba cha wageni maarufu ‘VIP Room’, ili
wapate angalau vinywaji kidogo huku akiwa nao.
Baada ya mjadala kidogo, viongozi walikubali
kuteremka, lakini Yaya akawa wa kwanza kuweka msimamo kwamba hatateremka.
“Safari yetu ilikuwa nzuri sana, ila tulipofika
Benin kidogo kukawa na vituko kidogo. Waziri mmoja wa serikali ya nchi hiyo
alisema tushuke, lakini ilikuwa vigumu kwa Yaya ambaye alisisitiza kwamba
anafuata ratiba.
“Kweli ratiba yetu pale ilikuwa ni kuweka
mafuta tu, unajua hata hiyo ndege tumeikodi pale. Nafikiri waziri huyo aliona
vizuri kuwaona wachezaji hao, lakini Yaya hakushuka hali iliyofanya viongozi
wabadili msimamo na kusema kushuka au kutoshuka ni uamuzi wa wachezaji wenyewe.
“Kweli wengine wakashuka, wengine baadhi
nafikiri watatu au wanne akiwemo Yaya wakabaki kwenye ndege,” alisema Aziz
Alibhai ambaye alikuwa kwenye msafara huo.
Akiwa jijini Dar, Yaya aligoma kutoka chumbani
asubuhi siku ya mechi dhidi ya Taifa Stars na kutaka apelekewe kifungua kinywa
chumbani.
Hata juhudi za kocha Sabri Lamouchi zilikwama
kumtoa chumbani baada ya kusisitiza alikuwa ana ‘focus’ (anafikiria chakufanya
katika mechi ya siku hiyo).
SOURCE: CHAMPIONI







hahahaaaah watu wanawapenda nyota hao, lakini nyota hao wamejisahau kuwa kazi yao ni ya kuburudisha watu
ReplyDelete