Iniesta akiwa na Casillas.. |
Pamoja na kwamba
wengi wamewahi kuzungumza, kiungo nyota wa Barcelona, Andres Iniesta naye
amefunguka.
Iniesta
amefunguka na kusema kocha wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho ameharibu
soka la Hispania.
Iniesta amesema
kuna mambo mengi yamefanyika wakati wa kocha huyo hayakusaidia soka la nchi
hiyo.
Lakini ajabu,
Iniesta hakutaka kuendelea kufafanua baada ya kuombwa na waandishi kufanya
hivyo, mwisho akasisitiza.
“Inawezekana
sijaeleweka, lakini sijisikii kulizumgumzia hili.”
Upande mwingine
inaonekana ni kama sehemu ya kumuunga mkono rafiki yake, Iker Casillas
aliyekuwa katika mgogoro mkubwa na Mourinho ambaye alimuweka benchi kwa zaidi
ya mechi 20.
0 COMMENTS:
Post a Comment