Kutembea
kwingi, kuona mengi, leo nilisafiri kwa saa tatu na nusu kutoka mji wa
Freiburg kuja hapa Weisbaden.
Lengo ni
kuwatembelea rafiki zangu, Mmoja ni Veronica aliyewahi kufanya kazi Global
Publishers nami kwa muda wakati aiwa nchini Tanzania.
Alisisitiza
nisiondoke Ujerumani bila ya kuwaona, yeye na washikaji zake wengine ambao ni
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mainz kasoro Sarah (dada wa kulia kwangu),
tulijumuika na kucheza mchezo uitwa Crockett, si cricket.
Sijawahi hata
kuuona, hakika ni mzuri na nimeahidi nikirudi Tanzania ntaendeleza kasi.
Mwepesi lakini
unahitaji akili sana na mwisho unaondoa hata uchovu. Inawezekana tukajifunza
vitu vingi kupitia michezo, si lazima soka.
Naendelea kubaki
hapa Weisburg kwa siku moja kabla ya kutembelea Mainz kwa nusu siku, baadaye
nitarudi Frankfurt ambacho ni kituo cha mwisho.
Kabla ya kwenda kucheza walinipitisha mitaani kwanza...hapa ni saa mbili usiku..mwanga usikupoteze maana ndiyo kawaida hapa Ujerumani kwa kipindi hiki |
Hakika kutembea
kwingine ni kuona mengi, ingawa hii si safari yangu ya kwanza hapa Ujerumani,
lakini safari hii nimejifunza mambo mapya tena.
Nashukuru sana
Vero, Sarah, Rajos na washikaji wengine kwa ukarimu wenu nikiwa hapa Weisburg,
moja ya miji inayovutia kabisa ya Ujerumani.
Danke.
safi sana rafiki yangu! nimefurahi sana kukukaribisha hapa ujerumani, natumaini kwamba umefika salama nyumbani, karibu tena! salamu nyingi Sarah
ReplyDelete