Henrik
Larsson ameweka rekodi ya aina yake baada ya kucheza na mwanaye akiwa na umri we
miaka 41.
Larsson
amecheza timu mmoja ya daraja la nne nchini Sweden inayojulikana kwa jina la Hogaborg
akiwa na mwanaye Jordan mwenye umri wa miaka 15.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa Celtic, Manchester United na Barcelona aliamua kupasha viatu vyake baada ya
kutocheza soka kwa kipindi kirefu.
Uamuzi
wake wa kucheza ulitokana na kwamba yeye ni kocha msaidizi lakini asilimia
kubwa ya wachezaji wake tegemeo walikuwa majeruhi, hivyo akaamua kuingia na
kusaidia.
Mwisho
timu hiyo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 na kufanikiwa kujiweka
katika nafasi nzuri ya kuepuka kuteremka.
Jordan
naye alifanikiwa kufunga bao moja na kutoa msaada mkubwa kuisaidia timu hiyo
kufanya vizuri siku hiyo.
Larsson
alisema inawezekana angefurahi sana kama angempa pasi mwanaye ili afunge na
kuahidi siku moja atafanya hivyo.
Wakati
akiwa anaichezea Celtic ya Scotland, Larsson alikuwa akienda uwanjani na
mwanaye huyo ambaye pia alikuwa akivaa jezi za timu hiyo zenye rangi ya kijani
na nyeupe.
Akiwa
na miaka 15, tayari Larsson ameshapata nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya
Sweden chini ya miaka 16.
0 COMMENTS:
Post a Comment