June 20, 2013




Wabunifu maarufu wa mitindo ya mavazi Domenico Dolce na Stefano Gabbana wameahidi kukataa rufaa leo au kesho mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi 20 gerezani.

Wawili hao wanaotumia kampuni maarufu ya ubunifu wa mavazi ya Dolce&Gabana wamekumbana na kifungo hicho kutokana na kukutwa na hatia ya kukwepa kodi.


Jana katika Mahakama ya jijini Milan, walipatikana na hatia ya kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia pauni bilioni moja kuanzia mwaka 2004.

 


Kabla ya kutoa huku, mahakama ilisema walikuwa wakitumia kampuni moja nchini Luxenbourg ili kukwepa kodi hivyo wanawatia hatiani.

Hata hivyo, wakali hao wa ubunifu wa mitindo ya mavazi wamesisitiza watakata rufaa ili kupinga hukumu hiyo.


Watu mbalimbali maarufu wamekuwa wakivaa nguo au kutumia vipodozi vinavyotengenezwa na wawili hao.

Baadhi ya watu maarufu wanaojulikana zaidi kwa kutumia vifaa vya Dolce&Gabana ni Madonna, Naomi Campbell na Katy Perry.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic