Uamuzi wa Barcelona, kumsajili nyota Neyma kutoka Santos ya Brazil umeonywa kwamba unweza ukaharibu mambo hapo baadaye.
Kocha na mchezaji wa zamani wa timu hiy, Johan Cruyff amesema kuna nafasi kubwa ya Messi na Neymar kuingia katika mgogoro.
Cruyff raia wa Uholanzi amesema wachezaji hao ni kama manahodha na ni nadra wote kuongoza mashua moja.
Kauli yake imeungwa mkono na wadau kadhaa ambao wanaamini baadaye kutakuwa na tatizo.
Hata hivyo wako ambao wanaamini kama kila mmoja ataachana na kuona ni maarufu zaidi, basi Barcelona itafaidika zaidi.
Lakini Neyma ameishasema atamsaidia Messi kuendelea kuwa mchezaji namba moja duniani, ingawa inaonekana upinzani wan chi zao katika soka unaweza kusababisha upinzani kati yao.
Messi ndiye mchezaji anayependwa zaidi nchini Argentina wakati Neymar ni kipenzi za Wabrazil.
0 COMMENTS:
Post a Comment