June 5, 2013

Na Saleh Ally, Freiburg, Ujerumani
Vijana sita wa Kitanzania wanaoendelea kujifua nchini Ujerumani chini ya Fels Project sasa wamedishwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa ndani.

Ndani ya uwanja wa ndani ambao nyasi zake ni rangi ya bluu, wachezaji hao wamekuwa wakiendelea na mazoezi kama kawaida kama inavyokuwa katika uwanja wa nje.



Lakini tofauti ni kwamba hata kama nje kunakuwa na mvua au hali ya baridi, wenyewe wanaendelea kuona ni hali ya kawaida kwa kuwa kuna mitambo maalum kwa ajili ya kutengeneza hali ya joto.


Wameendelea na mazoezi hayo chini ya mwalimu mkongwe anayejulikana kwa jina la Laex na jana walicheza na watoto mbalimbali katika eneo la klabu hiyo iliyo chini ya Alington.

Chini ya Fels Project, vijana hao wataendelea kujifunza mambo mbalimbali ya ndani na nje ya uwanja.


Mfano, zaidi ya mara tatu kwa wiki wamekuwa wakiingia darasani na kujifunza Kingereza kwa ajili ya mawasiliano, lakini namna ya kufanya usafi na mambo mengine mbalimbali.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic