Kocha aliyemaliza muda wake na Real
Madrid, Jose Mourinho amesema hakumpanga kwa makusudi kipa Iker Casillas katika
mechi za kumaliza msimu.
Mourinho amesema alijua Casillas
alipania kucheza mechi hiyo, lakini akamuweka nje akijua wazi mashabiki
wangeshangilia sana kurejea kwake, kitu ambacho hakutaka kitokee.
„Ulikuwa ni uamuzi sahihi na
nilifurahishwa na nilichofanya,“ alisema Mourinho.
Casillas aliumia siku nne kabla ya mechi
hiyo, lakini akarejea mazoezini na kufanya vizuri lakini bado kocha huyo Mreno
aliyekuwa na ugomvi naye hakumpanga.
Mourinho na Casillas wamekuwa katika
ugomvi kwa muda mrefu hali iliyosababisha Mourinho achukue uamuzi wa kumtumia
kipa wa pili Diego Lopez katika mechi zake zote zikiwemo za Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment