KIUNGO wa Barcelona, Cesc Fabregas
ametamka kuwa hana mpango wa kuihama timu yake ya sasa licha tetesi kuendelea
kusambaa kuwa anawaniwa na timu za Ligi Kuu England ‘Premier’.
Fabregas ambaye ni mchezaji wa zamani
wa Arsenal amekuwa akiwaniwa na Manchester United na City kutokana na kutokuwa
na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona.
Kiungo huyo ambaye alifunga mabao 14 katika
msimu uliomalizika amesema: “Nina furaha kuichezea Barca, nataka kuendelea
kubaki hapa kwa miaka mingi zaidi.”
Barcelona ililazimika kumtumia Fabregas
kuwa mshambuliaji wa kati kutokana na Lionel Messi kuwa majeruhi, lakini ujio
wa Neymar unamaanisha kuwa Fabregas atarejeshwa kwenye nafasi yake ya kiungo.
0 COMMENTS:
Post a Comment